Serikali yakoleza kasi ya kuyaendea mageuzi makubwa ya elimu

NA MATHIAS CANAL

SERIKALI imesema kuwa, imeamua kufanya mageuzi ya elimu ambapo kufikia mwezi Disemba 2022 rasimu ya mitaala mipya pamoja na rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Julai 25, 2022 wakati akizugumza kwenye jopo la mjadala katika kikao cha Kikosi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya elimu duniani uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Serikali ya Tanzania imejipanga vyema na kufikia mwezi Januari mwaka 2023 inatarajia kuanza mchakato wa kufanya maamuzi baada ya rasimu hiyo kuwa imekamilika.

Pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Elimu wa Namibia, Mhe. Ester Anna Nghipondoka, Naibu Waziri wa Elimu Bosnia na Herzegavina, Adnan Husic, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Katibu wa Tume ya Kitaifa ya Elimu ya Qatar ya Utamaduni na Sayansi,Ali Al-Marafi.
Mchakato wa mageuzi ya elimu nchini Tanzania ulitokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili 2021 kuhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu na muelekeo mpya katika sekta ya elimu aitakayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news