SIKU MAHTMA GANDHI ALIPOMWANDIKIA BARUA ADOLF HITLER ASITISHE VITA YA PILI YA DUNIA MWAKA 1939


Huko Wardha,

India,

23/7/1939.
Rafiki yangu,
Marafiki wameniomba nikuandikie barua ili wewe uwe na ubinadamu.

Lakini nimekataa ombi lao,sababu nimehisi kwamba barua yoyote kutoka kwangu itakuwa sio ya heshima kwako.

Kitu ninachoona ni kwamba sio lazima nikuhukumu au nitatue hili tatizo na kwamba nimefikiria itakuwa ni vema nikikueleza.

Ni wazi kwamba wewe kipindi hiki ni mtu ambaye duniani unaweza kuzuia hivi vita,ambavyo vitapunguza upotevu wa binadamu kwenye mataifa makaidi.

Kwani hivi ni lazima wewe kulipa gharama kwa kitu ambacho kinaonekana kina haki na karama kwako?.

Je! Utaweza kusikiliza ombi la mtu ambaye kwa makusudi anakwepa mbinu za vita bila ya kuzingatia matokeo?.

Haina shida,natarajia unisamehe kama nimekukosea kwa kukuandikia hivi.


Herr Hitler. Nabakia,

Berlin. Rafiki yako mpendwa,

Germany. M.K. Gandhi

Post a Comment

0 Comments