Tanzania Commercial Bank yashiriki Maonesho ya 46 ya Biashara Sabasaba

NA DIRAMAKINI

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imeshiriki maonesho ya 46 ya Biashara Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa katika kuongeza matawi kila mkoa na wilaya ili kusogeza huduma kwa wateja wake.
Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Joanitha Deogratias (wa pili kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo.
Afisa Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Cornel Mlay (kulia), akizungumza na mmoja ya mteja alietembelea banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Katikati ni Afisa Uwendeshaji wa Benki hiyo, Godbright Mlay.

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa benki hiyo, Joanitha Deogratias alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.
Afisa Uendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Salha Singano (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa mmoja ya mteja alipotembelea Banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Kushoto ni Afisa wa Kitengo cha ICT, Joseph Bukuru.
Meneja Uhusiano wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Shilla Senkoro (kushoto), akizungumza na mteja kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo.

“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wale wakubwa pia mikopo kwa wastaafu kwa ajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo za kiuchumi,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news