VETA Chang’ombe yagudua dawa asili mkombozi kwa wakulima

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Chang’ombe imegudua dawa za asili ya kupulizia na kuua wadudu na kuondoa magugu shambani.
Akizungumzakatika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), Mwalimu wa Chuo cha VETA Chang’ombe, Ally Issa amesema, katika kukabiliana na wadudu waharibifu mashambani wameamua kubuni dawa hiyo ya asili ambayo itaweza kuondoa chagamoto inayowakumba mashambani wakulima.

"Wakulima wamekuwa na changamoto mbalimbali katika kilimo ikiwemo ya kuharibika kwa mazao mashambani, hivyo kupitia dawa hii ya asili ya wataweza kupuliza na kuua wadudu na kuondoa magugu shambani,"amesema.

Amesema, dawa hiyo ni mkombozi kwa wakulima na inapatikana kwa urahisi kwani imebuniwa na wazawa kutoka VETA.

Ameongeza kuwa, dawa hiyo ipo katika uangalizi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika hatua ya mwisho wakiwa wamepata cheti cha uchunguzi na kibali cha muda cha maonesho ikiwa tayari itaingia sokoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news