Waziri Mkuu aongoza kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Melia Mkoa wa Kaskazini Unguja jijini Zanzibar leo Julai 30, 2022. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mwenza wa kikao hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Mhe. Jenista Mhagama akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Mhe. Anne Makinda akizungumza wakati wa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa pamoja na Mtakwimu Mkuu Zanzibar Bw. Salum Kassim Ali wakifuatilia kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), Mhe. Hamza Hassan Juma akizugumza wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia hoja wakati wa kikao.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Post a Comment

0 Comments