Waziri Nape:Lengo tutunge sheria itakayokaa muda mrefu,itakayokubalika na pande zote mbili

NA DIRAMAKINI

WAZIRI WA Habari Mawasiliano ya Habari na Teknolojia Mheshimiwa Nape Nnauye amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufanya maboresho makubwa katika sekta ya habari nchini.
Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 kando ya mkutano wa wadau wa maendeleo uliofanyika New Africa Hotel (Four Points by Sheraton Dar es Salaam) jijini Dar es Salaam ambapo ameufungua.

"Tunatambua mchango wa wadau wa maendeleo katika kusaidia ukuaji wa vyombo vua habari nchini upashaji habari, matumizi ya teknolojia katika nchi yetu. Lakini pili tunaendelea kusisitiza commitment ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha tunaendelea kuboresha mazingira ya wanahabari, na habari na upatikanaji wa taarifa katika nchi yetu.

"Mtaona nimegusia kwamba mchakato wa kupitia sheria, kanuni unaendelea vizuri, lakini pia tunapitia na sera ya habari kwa sababu hapa ni mambo matatu kwa pamoja. Nimeona hapa watu wengi wanazungumzia zaidi sheria, lakini sheria inatengenezwa na sera, na sera inatengeneza sheria na sheria kanuni, hivi ni vitu vitatu vinategemeana,"amesema Waziri Nape.

Ameongeza kuwa, "Kwa hiyo tuko katika mchakato mzuri tunaendelea vizuri tunawashukuru wadau wa maendeleo kwa jinsi wanavyoshiriki katika kujadiliana, kubadishana mawazo na kuona namna ambavyo tunafanya sekta zetu na nchi yetu kuhakikisha inaendelea mbele zaidi. 

"Ndio tumo katika mazungumzo nao na baada ya pale na wenyewe wanafuraha kwamba wameleta maoni yao na sisi tumeleta ya kwetu tunajadiliana.

"Tunazungumza tuone namna ambavyo tutaboresha, nimewahi kusema na hapa nataka nirudie, sheria ya habari ilipotungwa ililenga kutatua matatizo katika sekta ya habari, ikiwemo matatizo ya ajira zao, maslahi yao, mazingira yao ya kazi, haki zao, wajibu wao, sasa inawezekana masuluhisho yaliyowekwa kwenye sheria ndio yanayogombaniwa kwamba ndio sahihi au sio sahihi.

"Sasa katika mazingira hayo Serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuleta mbadala wa yale yanayolalamikiwa tukae mezani tuzungumze nao.Mchakato hauwezi kuwa mfupi na mchakato wa mazungumzo mimi nimeukuta, tutaendelea nao tunaangalia namna ya kuukamilisha mapema kadri inavyowezekana, tutakakubalina na tutakamilisha. 

"Lengo tutunge sheria itakayokaa muda mrefu, lakini sheria itakayokubalika na pande zote mbili,lakini sheria itakayotengeneza mazingira mazuri na bora zaidi kuliko tuliyonayo,"amesema Mheshimiwa Waziri Nape. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news