106,295 watuma maombi kujiunga vyuo 76 vilivyoidhinishwa na TCU

NA DIRAMAKINI

ZAIDI ya waombaji 106,295 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 76 vilivyoidhinishwa kudahili na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) huku programu 757 zikiruhusiwa ikilinganishwa na programu 724 mwaka 2021/2022.
Katibu Mtendaji Mkuu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa ameyasema hayo leo Agosti 24, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.

Amesema, kwa mwaka huu kuna jumla ya nafasi 172,168 ikilinganishwa na nafasi 164,901 mwaka uliopita. Hii ni ongezeko la nafasi 7,267 sawa na asilimia 4.4 katika programu za shahada ya kwanza.

“Katika mwaka wa kwanza ya udahili, Jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 ya waombaji wote walioomba udahili wameshapata udahili vyuoni,"amesema Prof.Kihampa.

Aidha, amesema mwenendo wa udahili wa awamu ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitano (2018/2019 hadi 2022/2023) unaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria ongezeko la wahitimu wa kidato cha Sita na wale wa Stashahada.

“Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa,"amesema Kihampa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news