Azam FC, ZESCO United watoka sare AZAMKA

NA DIRAMAKINI

MCHEZO wa kirafiki kupitia Tamasha la AZAMKA mahususi kwa timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam ulitamatika baada ya wana lambalamba Azam FC kutoa sare ya sufuri kwa sufuri na ZESCO United ya Zambia.

Hayo yamejiri Agosti 14, 2022 katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo lilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo kutoka kwa staa wa bongo fleva, Ray Vanny ambaye alitinga dimbani hapo na gwaride maalumu.

Post a Comment

0 Comments