BRELA yatoa wito kwa wafanyabiashara

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Andrew Mkapa amewataka wafanyabiashara kurasimisha biashara zao BRELA ili kuzipa ulinzi wa kisheria.
Bw. Mkapa ametoa rai hiyo mapema leo wakati akihojiwa katika studio za redio Arnuur ya Jijini Tanga.

Bw. Mkapa amesema mfanyabiashara anaporasimisha biashara yake inakuwa ni rahisi kupata fursa mbalimbali za kibiashara ikiwa ni pamoja mikopo kutoka taasisi za fedha na zabuni mbalimbali zinapotangazwa.
Aidha amewataka wafanyabiashara kutambua kuwa Leseni za Biashara kundi A zinazotolewa na BRELA zinahusu biashara zenye sura ya kitaifa na kimataifa na kwamba zinaweza kufanywa mahali popote tofauti na leseni za Biashara kundi B zinazotolewa na Halmashauri ambazo zinatumika katika halmashauri husika na si vinginevyo.
Maafisa wa BRELA wako mkoani Tanga kutoa mafunzo kwa Maafisa Biashara wa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Post a Comment

0 Comments