LIVE:YANGA SC vs VIPERS SC-UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFURIKA

Hii ni mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Vipers SC. Mgeni rasmi wa shughuli ya leo ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (Bara), Abdulrahman Kinana.

Mashabiki wa Yanga walianza kuwasili uwanjani ilikuwa ni kuanzia majira ya saa 1:00 asubuhi huku tiketi zikiisha mapema.

Nyota wa Yanga,Bernard Morrison amesema kuwa ni muhimu kwa mashabiki kuweza kujitokeza kwa wingi kuona namna hali itakavyokuwa.

“Jamani jamani njooni kwa wingi jamani,tupo vizuri na tunajua kwamba kuna mambo mengi ambayo tumeyaandaa kwa ajili yenu,”.

Pia Kocha Mkuu wa Yanga,Nasreddine Nabi amesema kuwa wakati wa Yanga kushuhudia burudani ni leo.

Post a Comment

0 Comments