Mfalme wa Saudi Arabia apokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa Rais wa Zambia

NA DIRAMAKINI

MSIMAMIZI wa Misikiti Mitakatifu Miwili Mitakatifu na Mfalme wa Saudi Arabia,Salman bin Abdulaziz Al Saud amepokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema, kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Ujumbe huo umepokelewa na Prince Faisal bin Farhan bin Abdullah ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, alipokutana Agosti 7, 2022 jijini Riyadh katika Wizara ya Mambo ya Nje na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zambia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Stanley Kakubo.

Katika mkutano huo,wawili hao walijadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na njia za kuyaboresha katika nyanja mbalimbali, pamoja na masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yenye maslahi mapana kwa pamoja.
Mhe. Kakubo alisisitiza dhamira ya Zambia ya kuendelea kushirikiana na watu na Serikali ya Ufalme wa Saudi Arabia katika nyanja mbalimbali za ushirikiano wa pande mbili na wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na amani na usalama, pamoja na biashara na uwekezaji, kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia alipongeza uhusiano wa muda mrefu ambao unaendelea kuwepo kati ya nchi hizo mbili na alisema wataendeleza ushirikiano kati ya Ufalme huo na Zambia, pamoja na msaada katika ngazi zote za ushirikiano.
Mawaziri hao wawili waliahidi kuendelea kufanya kazi kwa karibu na kuhakikisha mahusiano hayo yanadumishwa zaidi kwa manufaa ya mataifa hayo na raia wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news