Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika sala ya Ijumaa, amtembelea mwanasiasa mkongwe Mzee Khamisi Abdulla Ameir

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar,Mhe.Haroub Ali Suleiman, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar, Mhe. Said Salim Al-sinawi, alipowasili katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo Agosti 12, 2022.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja jijini Zanzibar leo. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Khamisi Abdulla Ameir aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Maisara kumtembelea na kumjulia hali yake. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu kinachoelezea Historia ya Maisha yake Mzee Khamis Abdulla Ameir, aliyewahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo alipofika nyumbani kwake Maisara Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kumjulia hali yake leo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mzee Khamis Abdulla Ameir, aliyewahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Maisra Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kumtembelea na kumjulia hali yake leo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma Kitabu kilichoandikwa na Mzee Khamis Abdulla Ameir, kinachozungumzia historia yake, baada ya kukabidhiwa wakati wa mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kumtembelea na kumjulia hali yale leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news