Rais Dkt.Mwinyi amtembelea mwanasiasa mkongwe,Mzee Ali Ameir Mohammed

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mzee Ali Ameir Mohammed alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja kumtembelea na kumjulia hali yake leo Agosti 7,2022.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Ali Ameir Mohammed alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumtembelea na kumjua hali yake na kushoto kwa Rais ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassam Othman Ngwali.(Picha na Ikulu).Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali (kushoto kwa Rais) ya kumuombea Mzee Ali Ameir Mohammed (kulia) aliyekuwa Mbunge wa Donge, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani, kumtembelea na kumjulia hali yake.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu na Mzee Ali Ameir Mohammed, kinachozungumzia historia ya Vyama vya TANU na ASP, kabla ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),kitabu hicho ameandika yeye kwa ajili ya historia ya Vizazi vijavyo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Ali Ameir Mohammed, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Donge, Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja kumjulia hali yake leo na kushoto kwa Mzee Ali ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mzee Ali Ameir Mohammed baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo baada ya kumtembelea na kumjulia hali yake.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news