Rais Dkt.Mwinyi awaapisha viongozi mbalimbali leo Agosti 5

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi na watendaji mbalimbali wa Serikali kushika nyadhifa zao kufuatia uteuzi aliofanya hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha, Rajab Yussuf Khamis Mkasaba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja,kabla Mkasaba alikuwa mwandishi wa habari wa Rais, hafla hiyo imefanyika leo ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Katika hafla hiyo iliofanyika ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Juma Makungu Juma kuwa Naibu Waziri Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi pamoja na Masoud Hussein Idd kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu.

Aidha, Dkt.Mwinyi amemuapisha Dkt. Maua Abeid Daftari kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Rashid Ali Salim kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda pamoja na Rajab Yussuf Mkasaba kuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja.

Hafla hiyo ya kiapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Chama Cha Mapinduzi, akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said pamoja na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Abdalla Juma ‘Mabodi’.

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mawaziri, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, Meya wa Jiji la Zanzibar Mohamed Mahamoud Mussa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini pamoja na wanafamilia,

Post a Comment

0 Comments