Rais Samia ametupa heshima kubwa kupitia fedha za miradi ya maendeleo-Waziri Simbachawene

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi billioni 16 kwa mwaka uliopita wa fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo katika mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ukiwa na kauli Mbiu “Sensa ni Msingi wa Mpango wa Maendeleo. Shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya Taifa.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipata juisi katika banda la lishe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Watu wanahitaji kusikia shida zao zinazungumzwa, ni imani yangu kwamba viongozi tutaendelea kushirikiana na fedha yoyote ya mradi wa maendeleo itakayokuja tutaitumia vizuri,”amesema.

Waziri Simbachawene amepongeza timu ya wakimbiza Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanya kazi nzuri.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw.Sahili Geraruma akikagua barabara ya lami kilomita moja Mpwapwa Mjini kabla ya kuizindua. (Picha na OWM).

Mwenge wa uhuru umekimbizwa kwa umbali wa kilomita 100 na umezindua miradi miwili, miradi mingine miwili imewekwa jiwe la msingi na mradi mmoja kutembelewa yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 1.4.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news