Rais Samia asisitiza matumizi ya lugha ya Kiswahili

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula katika ukanda mzima wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuzisihi nchi hizo kuwekeza kwenye ‘Uchumi wa Buluu’.
Rais Samia amependekeza hayo katika Mkutano wa 42 wa SADC uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumzia uwiano wa kijinsia waliokubaliana katika ukanda huo, Rais Samia amesema Tanzania imejitahidi kutoa fursa kwa wanawake hasa katika nafasi za uongozi za kimkakati.

Miongoni mwa nafasi hizo za uongozi serikalini na bungeni ni pamoja na za uwaziri wa Ulinzi, Mambo ya Nje, Uwekezaji, Utalii pamoja na nafasi ya Spika wa Bunge.

Rais Samia alitoa maoni yake kwa lugha ya Kiswahili ikiwa ni jitihada za kuchapusha matumizi ya lugha hiyo miongoni mwa nchi za SADC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo Baada ya Mkutano wa Viongozi, Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Mji wa Kinshasa nchini DRC.(Picha na Ikulu).

Katika mkutano huo uliopitisha maazimio 27 Rais Samia amesisitiza uharakishwaji wa mchakato wa Kiswahili kupitishwa rasmi kama lugha ya nne ya Jumuiya ya SADC.

Mkutano huo wa SADC pia ulishuhudia makabidhiano ya Uenyekiti kutoka kwa Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera na sasa nafasi hiyo imechukuliwa na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi.

Rais Samia leo atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini DRC ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Felix Tshisekedi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news