Ruzuku ya Bilioni 100/- yapunguza makali bei ya mafuta, EWURA yatangaza bei mpya leo Agosti 3

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia leo Jumatano, Agosti 3, 2022.
Kwa mujibu wa EWURA, bei za mafuta katika soko la Dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia.

Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa Agosti 2022.

Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo, imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022 kama inavyooneshwa hapa chini;

Post a Comment

0 Comments