TANESCO:Hatuzimi tena LUKU, tutawaambia

NA DIRAMAKINI

MUDA mfupi baada ya Shirika la UmemeTanzania (TANESCO) kuwataarifu wateja wake kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa malipo ya kabla (LUKU), hivyo wateja kushindwa kununua umeme kwa muda wa siku 4 kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 22 hadi 25 Agosti 2022, muda wa saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi wamesitisha zoezi hilo.


Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 17, 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano na Masuala ya Umma TANESCO makao makuu jijini Dodoma.


Post a Comment

0 Comments