NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Oman zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za uwekezaji, elimu, uvuvi na utamaduni.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mulamula amesema kuwa ni wakati sasa kwa mataifa hayo mawili kuongeza ushirikiano katika sekta za uwekezaji, elimu, uvuvi na utamaduni kwa maendeleo ya mataifa yote mawili.
Nae Balozi wa Oman nchini, Mhe. Al Sidhani amesema kuwa Oman ipo tayari wakati wote kuwekeza katika maeneo yenye fursa hapa Tanzania.

“Naomba endapo Tanzania mtaona maeneo mapya ya ushirikiano hususan fursa za uwekezaji na biashara msisite kutushirikisha tukajadiliana na kuitekeleza azma hiyo kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Balozi Al Sidhani.
0 Comments