NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amewaasa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi kuwa wazalendo katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022 ili kuwa na takwimu sahihi zitakazoleta tija kwa Taifa.
Washiriki wa Mafunzo ya Sensa ngazi ya Wilaya wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu (hayupo pichani) alipotembelea kituo cha Yombo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 15, 2022. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Alisema kuwa, Serikali imewaamini kuwapa jukumu la kukusanya taarifa hizo hivyo hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa usahihi kwa kuzingatia weledi na uzalendo wa hali ya juu.
Aliongezea kuwa Serikali imelipa kipaumbeke suala la sensa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kulibeba jambo hilo kwa unyeti wake, maana linategemewa na taifa zima.
“Hatutaliangusha Taifa wala Mhe. Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan tupo tayari kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya nchi yetu,”alisema Joyce.
0 Comments