Viongozi, wananchi waendelea kumiminika banda la Benki Kuu maonesho ya Nanenane jijini Mbeya


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi, alipofika mapema leo katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, zawadi ya pochi ambazo pia hutumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji sahihi wa noti.
Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo akitoa elimu kuhusu Alama za Usalama za Noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya. Kulia kwake ni Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando.
Afisa Utawala Mwandamizi BoT, Bw. Dennis Alfred, akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Wachambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Hassan Mbaga na Bi. Laila Kisombe wakitoa elimu kuhusu namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau, akielezea namna BoT inasimamia mifumo ya malipo nchini kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news