WAZIRI DKT.MABULA ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA SENSA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki kikao cha Kamati Kuu ya Sensa kwa ajili ya kupokea taarifa ya Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika kuanzia Agosti 23, 2022.
Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kimefanyika tarehe 18 Agosti 2022 katika ukumbi wa kituo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa pili wa rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah pamoja na Mawaziri wa serikali ya Muungano na Mapinduzi.Katika kikao hicho Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwaeleza wajumbe wa Kikao hicho kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti 2022 iwe siku ya mapumziko.

Post a Comment

0 Comments