Waziri Prof.Mkenda:Msimamo wa Rais Samia kupitia Diplomasia ya Uchumi umeiwezesha Tanzania kupata dola milioni 925 kuboresha miundombinu ya elimu

NA MATHIAS CANAL-WEST

DIPLOMASIA ya Uchumi iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ndani na nje ya nchi imesaidia upatikanaji wa Dola za Marekani Milioni 925 kuboresha miundombinu ya elimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Kyela mkoani Mbeya tarehe 7 Agosti 2022.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo wilayani Kyela  tarehe 7 Agosti 2022 wakati akitoa maelezo kuhusu sekta ya elimu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa John Mwakangale wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Mbeya.

Waziri Mkenda amesema kuwa Dola Milioni 425 ni kwa ajili ya Mradi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano wa HEET ambao unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 425.0 sawa na shilingi bilioni 972.0 ambao ni Mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya uzinduzi wa miundombinu mipya na iliyokarabatiwa katika vyuo vya ualimu kupitia mradi wa UPC wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Rungwe katika mkoa wa Mbeya tarehe 7 Agosti 2022.

Prof Mkenda amesema kwa lengo kuu la Mradi wa HEET ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuandaa mitaala mipya na kuboresha mitaala ya programu za kipaumbele ili iendane na mahitaji ya soko la ajira na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Elimu ya Juu nchini.

Mradi huo umebainisha Programu 14 za Fani za Vipaumbele vya Taifa ambazo ni pamoja na: Uhandisi na Teknolojia; TEHAMA; Malighafi Asilimia za Kisayansi; Sayansi ya Afya; Mipango Miji, Mazingira na Teknolojia; Nishati Jadidifu; Rasilimali Maji; Mabadiliko ya Tabia ya Nchi; Kilimo na Kilimo Biashara; Hifadhi ya Wanyapori; Utalii na Ukarimu; Taaluma ya Viwanda; Insia; na Ualimu.
Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Tulia Ackson akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati wa ziara ya siku nne ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mkoani Mbeya tarehe 7 Agosti 2022.

Waziri Mkenda amesema kuwa Dola Milioni 500 ni mradi wa kuimarisha ujifunzaji shule za msingi uliofadhiliwa na benki ya Dunia ambapo utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano utaboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufunfishaji, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za utoaji huduma ngazi A halmashauri.

Kupitia mradi huo wa Boost shule 6000 nchi nzima zitatekeleza mpango wa shule salama, vituo vya walimu na shule za msingi 800 kiwekewa vifaa vya TEHAMA kwaajili ya kuwawezesha walimu kujifunza na utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu, madarasa 12000 ya Elimu ya awali kuboresha, uandikisha wa wanafunzi elimu ya awali kuongezeka.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza katika viwanja vya John Mwakangale wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kyela mkoani Mbeya tarehe 7 Agosti 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Tulia Ackson, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Me Juma Homera mara baada ya uzinduzi wa miundombinu mipya na iliyokarabatiwa katika vyuo vya ualimu kupitia mradi wa UPC ikiwa ni siku ya tatu katika ziara yake ya siku nne mkoani Mbeya tarehe 7 Agosti 2022.

Waziri Mkenda amesema kuwa Rais Samia amekusudia kuboresha sekta ya elimu na kupitia uongozi wake ulio bora ni wazi kuwa kwenye sekta ya elimu yajayo yanafurahisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news