Yanga SC yamaliza mkataba na Hassan Maulidi Bumbuli, awaaga

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeachana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli baada ya kumaliza mkataba wake.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 12, 2022 na Idara ya Habari na Uhusiano ya Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo,Bumbuli ameushukuru uongozi wa Yanga kwa hatua hiyo akisema; “Kwa dhati ya moyo Wangu NAWASHUKURU sana Wana Yanga, Hakika naweza kusema kwamba ni ninyi ndio mnafanya ukubwa huu Klabu ya Yanga.

“Inaweza kuhuzunisha kwamba leo nawaaga, naondoka uongozini, lakini nina furaha na shauku kwa Changamoto mpya mbele yangu, na pia nina shauku kuona mpya yaliyoandaliwa kwa ajili yenu na kwa Klabu yangu pendwa.

“Ni zawadi nzuri sana niliyopokea na kuifurahia kufanya kazi Yanga, kuwahudumia #Wananchi,”.

“Ahsanteni kwa kunionyesha wema na hekima, hakika mlifanya Yanga kuwa mahali nilipofurahia sana kutumia muda wangu za kazi na zaidi,”.

“Kwenu WanaYanga, sina la kusema, hii ni kwa sababu sipati maneno ya kuelezea jinsi ninavyowashukuru! Ninyi ni watu Maalum sana..

“Nimekuja tukiwa watupu vyote pesa na mataji, naondoka huku vikapu vikiwa vimesheheni na rekodi iliyowekwa kwa kishindo. Ahsanteni kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia,” amesema Bumbuli katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news