IJP Wambura atoa maagizo mawili kwa askari polisi

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IJP), Camillus Wambura amewataka askari wa jeshi hilo kuzingatia uadilifu na kutenda haki wakati wanapo wahudumia wananchi kwa kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya kulinda watu na mali zao.

IJP Wambura amesema hayo wakati akifungua Kituo cha Polisi Ngoyoni kilichopo Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo mbali na kutoa pongezi kwa wadau werevu waliofanikisha ujenzi wa kituo hicho pia amewataka wananchi kujiepusha na utengenezaji wa pombe ya moshi aina ya gongo, kujiepusha na matukio ya mauaji yanayotokana na migogoro ya ardhi sambamba na mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Simon Maigwa amesema kuwa, ujenzi wa kituo cha Polisi Ngoyoni hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 128 ambapo kitarahisisha utoaji wa huduma za Kipolisi kwa kushughulikia makosa mbalimbali ikiwemo uhalifu na wahalifu.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Assenga, Bi. Catheline Assenga amesema kama familia wameridhia kutoa kwa hiari eneo walilokuwa wakimiliki na kulikabidhi kwa Jeshi la Polisi ili kujenga kituo cha polisi kwenye eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news