Iliki imebeba utajiri mkubwa kiafya, inaweza kuipa figo, kibofu chako uhai

NA DIRAMAKINI

NI wazi kuwa, Mungu ametupa zawadi za kipekee sana hapa duniani, miongoni mwa vitu au zawadi hizo za asili zikitumika kikamlifu zimekuwa zikileta matokeo chanya katika miili na hata afya zetu.

Waafrika tunasifika kwa kuwa na vyakula na hata mimea ya asili ambayo imeendelea kuwa tiba lishe miaka na miaka na huwa inatibu magonjwa mengi tena sugu.

Mathalani, iliki ni moja ya kiungo ambacho wengi wetu tunakifahamu sana na huenda huwa tunakitumia karibu kila siku kwenye shughuli za mapishi ya jikoni hususani katika kuandaa chai, lakini licha ya kwamba ni kiungo tu pia kina faida zake kwa afya.

Wataalamu wa afya wanasema, matumizi ya iliki husaidia sana kuipa uwezo mzuri figo hususani wa kuondoa taka mwili ndani ya mwili.

Pia huwa inasaidia sana kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni, kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kuwasaidia wale wenye shida ya kukosa choo kwa muda mrefu.

Mbali na hayo, iliki imekuwa ikisifika sana kwa uwezo wake wa kusaidia kuweka sawa harufu ya kinywa, pamoja na kutibu shida ya vidonda vya mdomoni au matatizo yote ya kinywa na koo.

Pia iliki ina uwezo mzuri sana wa kutibu matatizo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo ikiwemo kupambana na magonjwa mbalimbali. Iliki inatajwa kuwa na msaada mkubw akatika kukabiliana na magonjwa ya saratani na shinikizo la damu.

Wakati huo huo, iliki pia ina uwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua sambamba na kikohozi, huku isifika kwa kuwa na uwezo wa kuimairsha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula pamoja na kuondoa maumivu ya viungo mwilini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news