Maafisa kujengewa uwezo juu ya sheria ya kazi

NA DIRAMAKINI

TAASISI ya Ussy Production imewataka maafisa utumishi, viongozi wa vyama vya wafanyakazi maafisa rasilimali watu pamoja na wafanyakazi wa taasisi na mashirika mbalimbali ya umma na binafsi kujitokeza katika semina ya kujengewa uwezo juu ya sheria ya kazi.

Semina hiyo itakayofanyika kwa siku moja Mkoani Morogoro imelenga kuwaongezea uwezo mawakili, viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na wananchi juu ya sheria ya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo wakili mwandamizi wa mahakama kuu ya Tanzania Profesa. Ussy Charugamba Amesema semina hiyo itafanyika tarehe kumi mwezi wa tisa mwaka huu katika ukumbi wa Kanisa la wanauflume uliopo Kihinda Manispaa ya Morogoro.

Alisema semina itaongozwa na mtoa mada nguli na Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mzombe Prof. Binamungu ambapo atatoa elimu ya sheria ya kazi.

“Kila siku lazima tujifunze kwasababu kuna mawakili wanaajiriwa kila siku ambao ni chipukizi ambao hawana uzoefu kupitia semina hii watapata uzoefu,"alisema.

Aliongeza kuwa semina hiyo pia itawasadia wananchi katika kuongeza uwezo wa namna ya kutafuta ajira pamoja na kufahamu haki zao wakiwa kazini.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro wameishukuru taasisi hiyo kwa kuandaa semina itayowasidia kuwaongezea uelewa juu ya sheria ya kazi kwani wengi wao wanafanya kazi pasipo kujua haki na wajibu wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news