Makamu wa Kwanza wa Rais:Tujipange upya kuijenga Sekta ya Utalii nchini

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema kuna haja ya kujipanga upya katika kujenga Utalii ili kwenda sambamba na mwelekeo wa Uchumi wa Dunia kupitia maendeleo ya Sekta hiyo Ulimwenguni.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Hoteli ya Park Hayyat Mjini Zanzibar, akihutubia katika Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani, yanayoadhimishwa Kimataifa, ifikapo tarehe 27 Septemba ya kila mwaka.

Amesema kuwa, hatua hiyo itasaidia kuijenga upya na kuikuza Sekta ya Utalii Nchini, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wa Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mataifa mengine mengi, kote Ulimwenguni.

Post a Comment

0 Comments