Raila Odinga asusia uapisho wa Dkt.William Ruto leo


Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya, Raila Odinga. (Picha na Getty Images).

Raila Odinga mwenye umri wa miaka 77, awali aliashiria kwamba iwapo angechaguliwa kuwa rais, basi ungekuwa mwisho wake madarakani.

Ukweli ni kwamba, umri wa Odinga umeendelea kusonga mbele na bila shaka halijawa jambo rahisi kwake kuendelea kusukuma gurudumu la siasa na umri wake.

Na baada ya Mahakama ya Juu zaidi kutangaza kuwa, Dkt. William Ruto alichaguliwa kwa njia ya haki,Odinga kupata nafasi nyingine ya kujaribu kukata kiu yake ya kuwa rais, itakuwa ni miaka mitano ijayo atakapokuwa na umri wa miaka 82. Hiyo itakuwa mara yake ya sita kuwa mgombea wa urais iwapo atachukua hatua hiyo.

Pia haitakuwa kazi rahisi kumuondoa William Ruto kwenye kiti hicho ambaye kikatiba bado atakuwa anaweza kugombea kwa muhula mwingine wa miaka mitano. 
 
Ikumbukwe kwamba hata kama Raila Odinga angeshinda urais katika uchaguzi huu ambapo William Ruto amethibitishwa kuwa mshindi na Mahakama ya Juu zaidi, angeweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza kushika madaraka akiwa na umri mkubwa zaidi. Hata hivyo, amesema leo Septemba 13, 2022 hataweza kushiriki katika hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule Dkt.William Ruto;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news