Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 29, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Saidi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Mheshimiwa Valentina Andrew Katema kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza Septemba 29,2022 mheshimiwa Valentina alikuwa Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news