WANANCHI WA SELUKA,NYABU WAAHIDIWA KUCHIMBIWA KISIMA CHA MAJI

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Maji imeahidi kuchimba kisima na kujenga tenki la maji kwa wananchi wa Kijiji cha Nyabu na Seluka katika Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma waliokuwa wanasumbulia na hadha ya ukosefu wa maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene akizungumza na Mzee Michael Mnubi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Wihenzele katika Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Seluka katika mkutano wa hadhara. Ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 unatarajia kugharimu aaidi ya shilingi million 45.
Waziri wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wihenzele katika Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Maneno matupu katika Wizara yetu ya Maji hatuyataki, tunataka wananchi wetu wapate maji ili dhamira ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan iweze kutekelezeka,”amesema Waziri.

Waziri ametoa muda wa siku 30 kwa RUWASA kurekebisha miundo chakavu ya maji katika vijiji vya Seluka, Nyabu na Wihenzele uwe umekamilika na maji yaanze kutoka.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe, Mhe. George Simbachawene amesema 2004-2005 serikali ilitoa millioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji: mtandao wa maji ukawekwa na pampu ya maji inayotumia dizeli ikawekwa sambamba na tenki la maji kujengwa lakini bado wananchi hawakupata maji.
Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Seluka Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Tulipata milioni 157 ya ukarabati wa miundombinu ya maji kwa ajili ya kurekebisha kisima cha maji na maeneo mabovu ambayo kazi hiyo ilifanyika. Katika kufufua kisima cha maji kinachotumia diesel, ilitokea changamoto ya kukosekana uwiano mzuri kati ya kiwango cha maji kinachopandishwa na uwezo wa jereta, ambayo nayo ilianza kusumbua,”amesema.

Naye Bi. Easter Mgonela mkazi wa Kijiji cha Seluka amesema, shida ya maji imesababisha ukatili wa kijinsia, ameomba serikali kutatua changamoto ya kukosekana maji haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news