Waziri Prof. Mkenda, Leila Mohamed wapokea taarifa ya awali ya maendeleo ya uchambuzi wa Sera ya Elimu

NA MATHIAS CANAL-WEST

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof.Adolf Mkenda pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Leila Mohamed Leo tarehe 12 Septemba 2022 wameshiriki kikao kazi cha kamati ya mapitio ya sera ya elimu.

Katika kikao kazi hicho, Mawaziri hao wamepokea taarifa ya awali ya maendeleo ya kazi ya uchambuzi wa sera ya elimu.

Timu hiyo inayofanya kazi jijini Dar es Salam inaendelea na uchambuzi wa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambapo Sera hiyo ilifuta Sera ya Elimu ya mwaka 1995.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapitia sera hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia bunge tarehe 22 Aprili mwaka huu jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments