DC:ELIMU YA MAAFA IPEWE KIPAUMBELE

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Basilla Mwanukuzi ameziasa Kamati za Maafa kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao ili kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea na kuweka mkazo katika maafa yanayoathiri maeneo ya Wilaya hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Semina ya Kujenga Uelewa juu ya Upuguzaji wa Madhara ya Maafa kutoka katika Wilaya ya Korogwe wakifuatilia hoja wakati wa semina hiyo.(Picha na OWM).

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 12, 2022 wakati akifungua semina ya siku tano ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii kwa wajumbe wa Kamati za Maafa Wilaya hiyo iliyohusisha Kata sita zinazoathiriwa na maafa ikiwemo Magoma, Foroforo, Kalalani, Dindira, Bungu na Kizara zilizopo Korogwe mkoani Tanga.

Semina hiyo iliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IMO) imewafikia zaidi ya wajumbe 50 kutoka katika Kata hizo ikiwemo Viongozi wa dini, Wazee Mashughuli pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Kujenga Uelewa juu ya Upuguzaji wa Madhara ya Maafa katika Jamii kwa wajumbe wa Kamati za Maafa kutoka katika Kata Sita ikiwemo Magoma, Foroforo, Kalalani, Dindira, Bungu na Kizara zilizopo Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya aliwaasa wajumbe hao kuendeelea kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu juu ya kujikinga na madhara yatokanayo na maafa ili kiuendelea kuwa na jamii iliyo salama.
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Dorothy Pantaleo akiwasilisha mada ya dhana ya maafa wakati wa semina hiyo.

“Yatumieni mafunzo haya kama nyenzo muhimu katika maeneo yenu kuhakikisha mnajilinda na maafa yanayoweza kujitiokeza katika maeneo yenu, kukabili maafa kunahitaji kujitolea kwa mtu mmoja mmoja ili kuwa na mazingira salama,”amesisitiza Mhe. Mwanukuzi.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamado akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Kanali Selestine Masalamado akieleza lengo la semina hiyo ni kutoa elimu ya masuala ya maafa kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Kijiji ikiwa ni moja ya jukumu la idara hiyo ili kuwa na uelewa mpana kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa.
Diwani kutoka Kata ya Kizara Mhe. Haji Kaoneka akichangia jambo wakati wa Semina hiyo.

“Idara ya Menejimenti ya maafa imekuwa ikiendesha semina hizo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuendelea kuwajengea uelewa wananchi kuhusu mzingo mzima wa menejimenti ya maafa unaohusisha kuzuia, kujiandaa kukabili, kukabiliana, kurejesha hali pindi maafa yanapotokea katika maeneo yao,”alisema Kanali Masalamado.
Mratibu wa maafa Wilaya ya Korogwe Bw.Wycliffe Massolwa akizugumza wakati Semina hiyo.

Aliongezea kuwa miongoni mwa maeneo yaliyofikiwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kuzingatia imekuwa ikikabiliwa na maafa mbalimbali yakiwemo ya uhalibifu wa mazao unaosababishwa na uvamizi wa wanyamapori(tembo), ukame, pamoja na mafuriko.
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamaji (IOM) Bw.Reuben Mbugi akizugumza wakati wa semina hiyo.

Naye Afisa Afya kutoka Wilaya ya Korogwe Bw. Majaliwa Tumaini alieleza mada kuhusu ugonjwa wa ebola aliiasa jamii kuona umuhimu wa kujilinda na kulinda wengine kwa kuzingatia madhara yatokanayo na ugonjwa huu.
"Lazima tuchukue tahadhari zote muhimu kwani ugonjwa huu upo nchi jirani, kila mmoja awe mlinzi wa wenzake huku tukifuatilia maelekezo yanayotolewa na Wizara husika na wataalam wa afya,” alieleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news