Kamanda afunguka sakata la kujinyonga kwa Katibu wa Kanisa la Feel Free akimtamani mke wa Mchungaji Masanja

NA MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lisema uchunguzi wa awali wa polisi kuhusu tukio la Katibu wa Kanisa la Feel Free linaoongozwa na Mchungaji, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) kujiua kwa kujinyonga umeonesha kwamba marehemu pamoja na mke wa Masanja hawakuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro ameyasema hayo leo Oktoba 4, 2022 wakati akieleza kuhusu uchunguzi wa jeshi hilo kufuatia tukio hilo ambalo limeibua hisia tofauti kwa wananchi.

“Ni kweli uchunguzi wa awali unaonesha mawasiliano yanaonesha huyo marehemu akiwa anaomba, akiwa anataka, anaomba mahusiano ya kimapenzi na huyu, tu ambaye inadaiwa ni mke wa Masanja.

“Ni kweli pia kabla ya tukio mke wa Masanja akiwa na mama mwingine walikwenda nyumbani kwa Marehemu kumueleza kwamba yule Mke hataki msg za namna ile na hataki mahusiano na yeye.

“Ni kweli pia yule mtu alifadhaika baada ya kuelezwa waziwazi kwamba yule ni mke wa mtu na hataki mahusiano nae, sasa mtitiriko wa visa hivyo unatoa nafasi ya kutokuwa na shaka na mazingira ya kifo kile.

“Bila shaka atakua amejinyonga kwa sababu mbalimbali za fikra zake au sababu nyingine yoyote lakini hata hivyo bado Jeshi la Polisi haliwezi likaishia kwenye ushahidi wa awali ambao umeonekana…. mwisho huwa ni kufanya uchunguzi wa kitaalamu,” amesema Kamanda huyo.

Post a Comment

0 Comments