Kwa Mkapa mambo Yeeeeeeeee, ni Simba na Yanga SC

NA DR.MOHAMED OMARY MAGUO

HUU ni utenzi wa salaam za heri kwa timu zetu pendwa za Simba na Yanga ambazo leo Oktoba 23, 2022 zinacheza katika mashindano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jijini Dar es Salaam.

Ni kupitia mtanange wenye mvuto na hamasa kubwa ambao utapigwa saa 11 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Ungana na Dkt. Mohamed Omary Maguo akupitishe katika salamu muhimu na maalum kupitia shairi;


1

Timu za Simba na Yanga

Kutazama me'jipanga

Ni Simba na pia Yanga

Zote nazishangilia


2

Wapo walotoka Tanga

Kwa Mkapa me'shatinga

Shabiki Simba na Yanga

Uwanja umefurika


3

Wapo waliojichanga

Bagamoyo ya Mapinga

Na pia kutoka Mwanga

Simba, Yanga shangilia


4

Hakuna mwenye kupinga

Ukweli kuubananga

Kwamba Simba na Yanga

Timu bora Tanzania


5

Beti tano nazifunga

Nakisubiri kipenga

Kwa Mkapa mambo shwanga

Yanga na Simba hoyeeeeeee!


MTUNZI

Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mshairi wa Kisasa
Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Post a Comment

0 Comments