Kwa moyo huu wa Rais Samia, kwa nini asipongezwe na kupewa tuzo ya heshima?

NA MWALIMU MEIJO LAIZER

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia anastahili pongezi na tuzo maalumu ya uongozi bora na uliotukuka kwa hili la kuridhia kuwalipa sehemu ya mafao yao waliokatwa na mifuko ya jamii waliofukuzwa kazi kwa ajili ya vyeti vyeki.

Nidhahiri kuwa, nchi hii imefunguliwa kwa upya na Rais Samia, Mwenyenzi Mungu amempa upendo wa namna ya kipekee, wenye kujali utu,heshima na thamani ya wengine kama alivyoleta matumaini mapya na furaha kubwa kwa wale wote waliogiswa na sakata la vyeti hivyo wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Suala la Vveti feki liliguza maisha ya watu wengi wakiwemo watumishi wenyewe wa umma na familia zao.

Ni dhahiri kuwa, wote walioguzwa na fukuza fukuza ya vyeti feki katika Serikali ya Awamu ya Tano iliweza kuathiri maisha yao, kwani tukumbuke kabisa watumishi hao walikua wanaendelea na kupambana na shughuli zao za kila siku katika ujenzi wa Taifa letu na familia zao pia.

Pia ni ukweli usiyofichika kuwa, watumishi walioathirika katika suala zima la vyeti feki kwa sehemu kubwa wameweza kutumikia nchi yetu katika nyanja mbalimbali za maisha yao ya kila siku.

Kwa ujumla wao, wote walitumika kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu hasa katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu, Sheria Nakadhalika.

Sote tukumbuke kutokana na kundi hili la watumishi wenye vyeti feki wametoa mchango mkubwa kwa nchi yetu jambo ambalo Rais wetu ameliona na kufanya uamuzi sahihi.

Uamuzi wa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika hili la watumishi wenye vyeti feki waliofukuzwa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano, ni kweli kabisa inadhihirisha kuwa rais wetu ni Muungwana kwa watu wake wote,

Rais Samia ni kiongozi mwenye upendo mkubwa kwa wananchi wake wote, Ni Kiongozi aliyesheheni hekima,busara na utu kwa wananchi wake wote na ni kiongozi anayethamini na kuheshimu mchango wa kila Mtanzania jambo ambalo limemfanya kuridhia kulipwa kwa watumishi wa vyeti feki.

Licha ya changamoto ya vyeti vyeki, ni dhairi kuwa watumishi hao waliweza kutimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuhakikisha kupitia nafasi zao wanawajibika ili kuwezesha mipango ya Serikali inafikiwa kwa wakati na kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hivyo, kwa namna ya kipekee ninaona kuna umuhimu na upekee wa Rais Samia kupewa pongezi na tuzo maalum ya uongozi uliotukuka kwa uamuzi sahihi hususani kwa kutambua na kuheshimu kazi kubwa iliyofanywa na watumishi hao.

Sote kama Taifa tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba Mbingu na Nchi aliyetujalia Taifa zuri la Tanzania na kutupa Rais ambaye amejawa na Upendo Mkubwa, Uzalendo Mkubwa kwa Taifa Letu, na Aliyejaliwa Hekima, Busara na Utu kwa Wananchi Wake.

Watanzania wote kwa pamoja tuungane kumuombea Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ili Mungu aweze kuendelea kumjalia afya njema na maisha marefu kwa masilahi mapana ya nchi yetu.

Imeripotiwa Na:-
Mwl. Meijo Laizer
MNEC MSTAAFU
WILAYA YA SIHA
MKOANI KILIMANJARO
0755898037

Post a Comment

0 Comments