Mheshimiwa Mgalu:Mama kaupiga mwingi, kavunja rekodi maeneo yote muhimu

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Kodi Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum mkoani Pwani,CPA Subira K. Mgalu ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo anayendelea kuifanya kwa ustawi bora wa jamii na Taifa.

"Leo nimepata fursa ya kufanya uchambuzi mdogo wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2021/2022 kulinganisha na 2020/2021.

"Kama taarifa ilivyowasilishwa na Serikali kwenye Kamati yetu ya Bajeti kwa maeneo machache tu natanguliza kusema Mama kaupiga mwingi, kavunja rekodi maeneo yote muhimu hakika Serikali yetu Awamu ya Sita inaendelea pale Awamu ya Tano ilipoishia, inapambana na uchambuzi wenyewe ni kama ifuatavyo;

"Mapato ya ndani pamoja na Serikali za mitaa hadi Juni 30, 2022 zimekusanywa shilingi bilioni 24,395.6 sawa na asilimia 95 la lengo la kukusanya shilingi Bilioni 25,691.7 wakati mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2021 makusanyo yalikuwa Bilioni 20,594.7 sawa na asilimia 85.6 ya lengo la kukusanya Bilioni 24,065.5.

"Hapa tafsiri yake kuna ongezeko la zaidi ya shilingi Bilioni 3,800.9 kwenye mapato ya ndani kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2022 zaidi ya mapato yaliyokusanywa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021,"amefafanua CPA Mgalu.

Pia amesema, makusanyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2022 walikusanya shilingi Bilioni 20,931.3 sawa na asilimia 96.1 ya lengo la kukusanya shilingi Bilioni 21,778.1 wakati mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni 2021 TRA ilifanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 17,624.4 sawa na asilimia 86.7 ya lengo la kukusanya bilioni 20,325.8.

"Hii tafsiri yake kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2022 TRA iliongeza makusanyo yake kwa zaidi ya Bilioni 3,306.9 kulinganisha mwaka wa fedha ulioishia 30 June 2021

"Ufanisi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha ulioishia 30 June 2022 zilikusanya Bilioni 889.5 sawa na asilimia 103 ya lengo la kukusanya Bilioni 863.9 wakati mwaka wa fedha ulioshia Juni 30. 2021 Mamlaka za Serikali za Mitaa zilofanikiwa kukusanya Bilioni 757.0 sawa na asilimia 92.9 ya lengo la kukusanya Bilioni 814.9

"Hii tafsiri yake Halmashauri ziliongeza makusanyo ya zaidi Bilioni 132.5 kulinganisha na kiwango kilichokusanywa na Mamlaka za Serikali za mitaa mwaka wa fedha ulioishia 30 June 2021,"amefafanua CPA Mgalu.

Kwa upande wa pesa za maendeleo kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2022, CPA Mgalu amesema, Serikali imefanikiwa kupeleka kwenye miradi shilingi Bilioni 11,554.6 sawa na asilimia 99.7 ya bajeti ya kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya kiasi cha shilingi Bilioni 11, 591.1 ukilinganisha na mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2021 ambapo Serikali ilifanikiwa kupeleka Bilioni 8,349.9 kwenye miradi ya maendeleo kutoka kwenye mapato ya ndani sawa na asilimia 92.5 ya lengo la kupelekea bilioni 9,023.2 kutoka mapato ya ndani.

"Kwenye hili kuna ongezeko la zaidi ya Bilioni 3,204.7 kwenye miradi ya maendeleo mwaka ulioishia Juni 30, 2022 kulinganisha na mwaka ulioishia Juni 30, 2021 ndio maana tunaona miradi mingi ngazi ya vijiji mpaka kata inatekelezwa na Miradi ya Kimkakati inaendelea vyema hakika pochi ya Mama inafunguka tena kwa mapato ya ndani. Hongera Rais Samia Suluhu Hassan,"amefafanua CPA Mgalu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news