Rais Samia aipongeza Simba SC kutinga hatua ya makundi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Simba baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Rais Samia ametuma salamu hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter akionesha kuthamini kazi kubwa Simba SC waliyofanya ya kuingia hatua na kupeperusha vema bendera ya nchi.

“Kongole Simba kwa ushindi wa bao 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya Premiero De Agosto ya Angola na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika. Nawatakia kila la kheri katika michuano inayofuata.”

Ni kupitia mtanange uliopigwa leo Oktoba 16, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,.

Simba SC wameingia katika hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-1 kufuatia ushindi wa 3-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola wiki iliyopita

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news