Al Hilal wazima ndoto za Yanga ndani ya dakika tatu

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Al Hilal kutoka nchini Sudan imezima ndoto za Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC kutinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Ni baada ya Yanga SC kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa katika dimba la Al-Hilal jijini Omdurman, Sudan.

Al Hilal walimaliza hesabu dakika ya tatu kupitia kwa Mohamed Abdel Raman baada ya mabeki wa Yanga SC kufanya makosa na kuifanya timu hiyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-1.

Ni kufuatia mechi ya kwanza ambayo ilifanyika katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Oktoba 8, 2022 kufungana bao moja kwa moja.

Safari ya Yanga SC inazimika licha ya kuonekana kucheza vizuri tangu mwanzo wa mchezo ila ilishindwa kuvunja rekodi yake ya kutinga hatua ya makundi kwenye michuano baada ya mwaka 1998.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news