Serikali yakusudia kufanya jambo kuhusu usomaji wa vitabu nchini

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema itafanya jitihada za uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe wakati akifunga tamasha la 31 la vitabu lililomalizika leo katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa sasa ni wakati wa kuendeleza ushirikiano na sekta binafsi ambao ni waandishi na wachapishaji katika kuhakikisha wanarejesha ari ya usomaji wa vitabu nchini.
"Kwa kweli niwapongeze kwa jitahada za kuhakikisha tamasha hili linafanyika japokuwa kuna mapungufu ambayo kwa ushirikiano tutaweza kuyatatua katika matamasha mengine yajayo," amesema Prof. Mdoe.

Prof.Mdoe amesema kuwa utamaduni wa usomaji nchini umeshuka kwa kiasi kikubwa hivyo lazima kuwe na mbinu za kuhakikisha unarejea kama ilivyo kawaida.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Habari na Machapisho Bw. Kwangu Masalu ameshukuru Uongozi wa PATA kuweza kuwashirikisha katika maonesho haya.

Amesema wataendelea kufanya kazi kwa karibu na PATA katika kuhakikisha kazi ya uandishi na uchapishaji inafanyika vizuri kwa weledi.
Maonesho yajayo yatakuwa makubwa ambayo yatasaidia katika uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini na Watanzania kupata fursa ya kusoma machapisho mbalimbali kutoka kwa wachapishaji binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news