Serikali yawaonya wachepushaji wa maji

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

NAIBU Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameonya wale wote wanaochepusha maji kwa ajili ya kufanya shughuli zao ikiwemo kumwagia mashamba na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa na Mawaziri wenzake wa wizara za kisekta wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Amesema hayo Oktoba 27, 2022 wakati kamati ua mawaziri nane wa wizara za kisekta za kushughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi ilipokwenda kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging,’ombe mkoani Njombe.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza maeneo maji yanapoanzia na kufuata sheria pale wanapotaka kutumia na kusisitiza wanaochepusha maji kiholea waache kuacha mara moja.

‘’Kuna utaratibu na siyo kama nazuia maji yasitume, lakini kuna Bodi ya Maji ya Mto Rufiji inafanya kazi vizuri na kuna taratibu zake ukitaka kumwagilia maji nenda ofisi zao na unapewa utaratibu na unakuwa mtanzania mzalendo.
“Wewe unayelima na kumwagia mazao yako ufanikiwe basi usiwe kikwazo kwa watumiaji wengine wa maji majumbani kwa sababu ukitaka kuyavuta yote shambani kesho yake mradi, majengo makubwa na usambazaji mabomba yenye thamani ya mabilionji ya fedha itakwama, wewe unachepusha maji kwenye chanzo yatafikaje kwenye matenki tuache kuchepusha maji,"alisema Maryprisca.

Aidha, alionya wananchi wanaolima ‘vinyungu’ kwenye vyanzo vya maji kuacha tabia hiyo na kueleza kuwa, mtu yeyote anayelima maeneo ya vyanzo maji ni adui namba moja wa zile jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu anasababisha maji kukauka na kusababisha miundo mbinu inayotolewa kwa ajili ya miradi ya maji kukosa thamani.
Kwa mujibu wa Maryprisca, shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ni mwiko na haviruhusiwi kwa kuwa zinasababisha maji kukauka huku lengo la serikali kupitia wizara yake likiwa kuendelea kupata maji zafi na salama.

Pia Naibu wa Waziri wa Maji aliwataka wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji na kuacha kabisa kufanya shughuli zozote za kibinadanamu kwa kuwa zinaweza kuharibu vyanzo hivyo alivyovieleza vinahitaji uoto wa asili ili viweze kuimarika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news