TAMISEMI QUEENS YAITAMBIA JKT MBWENI

Nahodha Msaidizi wa Tamisemi Queens Sophia Komba akijaribu kumhadaa mchezaji wa kati wa JKT Mbweni Zam zam Hamis (c) 'aliyenyoosha mikono juu, huku wachezaji wenzake wa TAMISEMI Queens Lilian Jovin (GS) na Asha Said (WD) wakiwa tayari kumsaidia katika pambano kali la ligi ya Netiboli Tanzania lililofanyika jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Tamisemi ilishinda mchezo huo magoli 52-37.
Moja kati ya heka heka katika goli la Mbweni JKT wakati Mchezaji Gloria Benjamin wa Tamisemi Queens akijaribu kuwahadaa wachezaji Zamzam Hamis (C), Jesca Ngisaise (GA) na Upendo Mpera (WA) huku mchezaji mwenzake Mersiana Samwel (GD) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo mkali na wa kusisimua kati ya Tamisemi queens na Mbweni JKT uliomalizika kwa Tamisemi kushinda kwa magoli 52-37, katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji Zamzam Hamis wa Mbweni JKT akijaribu kuukamata mpira uliorushwa na Jesca Ngisaise (GA) wa JKT Mbweni huku mchezaji Semeni Abeid (WA) naye akinyoosha mkono kuuwahi mpira huo katika mchezo wa Ligi ya Netiboli Tanzania uliochezwa jana mjini Morogoro ambapo Tamisemi ilishinda magoli 52-37.
Mchezaji Lilian Jovin (GS) wa Tamisemi akifunga mojawapo ya magoli yaliyoipa ushindi timu yake dhidi ya JKT Mbweni katika mchezo mkali na wa kusisimua uliochezwa jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Tamisemi ilishinda kwa magoli 52-37.

Post a Comment

0 Comments