Waziri Dkt.Tax ateta na Balozi Luteni Jenerali Mkingule

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), amekutana na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Mhe. Mkingule alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Mhe. Waziri na kumpongeza kufuatia uteuzi alioupata hivi karibuni na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

Mhe. Mkingule pia alipokea maelekezo kutoka kwa Mhe.Waziri Dkt.Tax tayari kuelekea katika kituo cha kazi nchini Zambia.

Post a Comment

0 Comments