'WE ARE ONE' yavunja rekodi ya Dunia uchangiaji damu mtandaoni saa 24

NA DIRAMAKINI

WAFANYAKAZI wa kujitolea kutoka Korea wameorodheshwa katika Kitabu cha GUINNESS WORLD RECORDS kwa kufanikisha zoezi la watu wengi kujisajili kama wachangiaji damu mtandaoni ndani ya saa 24.
Oktoba Mosi, mwaka huu kikundi cha vijana cha kujitolea cha ‘WE ARE ONE’ kilikamilisha maombi ya kuchangia damu mtandaoni kwa watu 71,121 waliojitolea kwa saa 24 ili kuvunja Rekodi ya Dunia.

Wachangiaji damu hao walikuwa tayari kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu ili kuondokana na upungufu wa damu unaosababishwa na UVIKO-10, ikiongozwa na We Are One ambalo ni Shirika la Vijana wa Korea linaloendesha kampeni ya kuchangia damu ya 'Life ON Youth ON'.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Kimataifa kuhusu Usalama na Upatikanaji wa Damu, iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo Juni 2022, uhaba wa damu umeathiri nchi zote wakati wa janga la UVIKO-19.

Pia mnamo Januari 2022, Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani lilitangaza kuwa Marekani inakabiliwa na tatizo la damu la kitaifa, ambao ni mbaya zaidi wa damu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kupitia 'Red Connect', matumizi rasmi ya simu janja ya uchangiaji damu ya Shirika la Msalaba Mwekundu la Korea, waliojitolea wote walikamilisha maombi ya kuchangia damu kwa saa 24 kuanzia saa 8:00 asubuhi tarehe 1:00 Oktoba hadi saa 8:00 asubuhi tarehe 2 Oktoba.

Hii ilikuwa ni takribani mara saba ya rekodi ya Dunia ya awali ya 10,217 (saa 8) iliyokuwa ikishikiliwa na India.

Bw. Junsu Hong ambaye ni Mkuu wa WE ARE ONE amesema, "Iliwezekana sio tu kwa sababu ya watu waliojitolea, lakini pia maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Korea wanaofanya kazi mstari wa mbele kutatua uhaba wa damu, na kampuni ya TEHAMA iliyounda mfumo bora wa maombi ya kuchangia damu.

"Kwa maana hiyo ina umuhimu mkubwa. Nanaamini UVIKO-19 inaweza kushindwa wakati sisi sote ni wamoja,"amesema.
Tangu kuzinduliwa kwake Julai 30, mwaka huu, WE ARE ONE imekuwa ikifanya kampeni ya 'kuchangia damu 70,000' tangu Agosti 27, mwaka huu. Hadi kufikia tarehe 11, jumla ya watu 43,811 walikamilisha uchangiaji damu, na inatarajiwa kukamilisha uchangiaji damu wa watu 70,000 ifikapo Novemba, mwaka huu.Soma rekodi kamili hapa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news