2025 Saudi Arabia kutoa magari yanayotumia umeme yaliyoboreshwa kuliko ya Marekani

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Viwanda wa Saudi Arabia (SIDF), Ibrahim Almojel amethibitisha kuwa mwaka 2025 Taifa hilo la Kifalme litatoa gari la kwanza la umeme lililoboreshwa zaidi, na uzalishaji utafikia magari 150,000 kila mwaka.
Picha na iStock.

Uthibitisho wa Almojel umekuja wakati wa mahojiano na Rotana Khalejeyah, ambapo amesisitiza kuwa Saudi Arabia ina uwezo wa kufikia hilo kutokana na msaada unaotolewa na Serikali na sekta binafsi ili kuamsha sekta hiyo huku akipongeza sekta ya uzalishaji magari nchini humo kwa uthubutu na ubunifu.

Pia amefafanua tofauti kati ya Lucid na Ceer, akibainisha kuwa Lucid ya Marekani inalenga zaidi katika sehemu ya magari ya kifahari pia inazingatia mauzo ya magari maalum ili kufikia soko la Ulaya na la ndani.

Amesema, kwa Ceer mtazamo tofauti kwani wataenda mbali zaidi na watazingatia magari yenye uwezo na ubora wa hali ya juu, na yale yanayojulikana na kasi ya juu, pamoja na yale yenye maisha marefu ya betri.

"Saudi Ceer itazingatia zaidi matumizi ya kila siku na magari yanalotumiwa zaidi," Almojel alisema, akibainisha kuwa Ceer itakuwa kampuni inayotoa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la sasa na la baadae kwa matumizi ya mazingira mbalimbali na maelezo kwa kina yatatolewa katika siku zijazo.

Kuhusu SIDF na sekta ya fedha za viwanda nchini Saudi Arabia, Almojel amesema kuwa, watafadhili kiwanda chochote ndani ya Ufalme huo, hata kama kinamilikiwa na mgeni, lakini kwa sharti kwamba mgeni huyo atoe thamani ya ziada kwa nchi.

Pia amesema mtaji wa mfuko huo imepanda kwa kasi kutoka Saudi Riyal (SR) bilioni 40. Aidha, mfuko huo umefikia malengo ya Dira ya 2030 mfululizo, hata kabla ya kuanzishwa kwa mkakati wa viwanda, mtaji umeongezeka kutoka Saudi Riyal (SR) bilioni 40 hadi hadi bilioni SR 105.

Almojel amedokeza kuwa, kilichotokea katika miaka kadhaa baada ya kuzinduliwa na kutekelezwa kwa Dira ya 2030 kwa upande wa uwekezaji na msaada kutoka kwa Ufalme ni kubwa kuliko kile kilichotokea katika miaka 45 iliyotangulia.

Pia amebainisha wakati wa mahojiano umuhimu wa kuchanganya vyanzo vya mapato, si mapato ya serikali, bali mapato kwa nchi kama uchumi.

Mkurugenzi huyo amsema kuwa, matarajio ya Dira ya 2030, ambayo sasa ndani ya miaka saba ni kuongeza mauzo ya nje maradufu kutoka katika msingi wa 2020 kwa takribani SR bilioni 168-169, kufikia zaidi ya SR bilioni 500 katika miaka saba katika mauzo yasiyo ya mafuta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news