Benki Kuu yatoa tamko kali kwa wanaojihusisha na biashara ya ukopeshaji bila leseni, wananchi watakiwa kukaa nao mbali

NA DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imebaini kuwa,kuna baadhi ya taasisi,kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya utoaji mikopo nchini bila kuwa na leseni.Jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga ameyabainisha hayo leo Novemba 24,2022 kama ifuatavyo;"Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha.

"Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (2) (a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 3018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua shilingi milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili.

"Sambamba na tangazo hili, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwaasa wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni.

"Aidha, orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilitolewa na Benki Kuu ya Tanzania na inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz,"amefafanua Prof.Luoga kupitia taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news