Jaji adakwa akipokea hongo Mji Mtakatifu

NA DIRAMAKINI
 
MAMLAKA ya Kukabiliana na Ufisadi nchini Saudi Arabia imemkamata jaji anayehudumu katika Mahakama ya Rufaa katika eneo la Madinah kwa kupokea hongo.

Chanzo rasmi cha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Nazaha) kimesema kuwa Ibrahim bin Abdulaziz Al-Juhani, jaji katika mahakama ya rufaa ya mkoa wa Madina alikamatwa akipokea Riyal (SR) 500,000 kati ya Riyal (SR) 4,000,000 alizoahidiwa kutoka kwa mwananchi, kwa ajili ya kutaka kutoa uamuzi wa mwisho katika kesi inayoendelea katika Mahakama Kuu katika mojawapo ya mikoa.

Viongozi hao walisema: “Taratibu za kisheria dhidi ya washtakiwa hao zinakamilishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni,"imeeleza sehemu ya taarifa yao.

Nazaha imethibitisha kuwa itaendelea kumfuatilia mtu yeyote anayetumia vibaya ofisi ya umma kujinufaisha au kuharibu masilahi ya umma kwa njia yoyote ile, na itaendelea kutumia sheria, bila kuvumilia ufisadi.

Post a Comment

0 Comments