Kada wa CCM Augustino Matefu aanika siri za Dkt.Bashiru

NA DIRAMAKINI

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Augustino Matefu amesema Novemba 17, mwaka huu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ally Kakurwa alisema maneo ya hovyo na ambayo hayakupaswa kutamka na mtu wa hadhi yake, hivyo atambue kuwa kuna ambao wanayafahamu mengi yamuhusuyo kuliko anavyojidhania.
 
Akiwa katika Mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Novemba 17,2022 mkoani Morogoro, Dkt.Bashiru Ally Kakurwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa mbunge aliwataka wakulima kushikamana ili waweze kufikisha ujumbe kwa wanaowaongoza.

Alisema, sauti ya wakulima iwatishe aliwowaita wanyonyaji na kama hawajafika kwenye hatua hiyo ya kuwa watu au kundi la kutisha wanyonyaji bado watakuwa hawajafikia malengo.
Matefu ambaye ni mwanasheria kitaaluma ameyasema hayo Novemba 22, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema,Dkt.Bashiru siku hiyo aliropoka maneno ambayo yalikuwa hayaoneshi ukada wake na mustakabali wa Tanzania na pia hayakuzi uhusiano kati ya mkuu wa nchi na taasisi zake. "Ninaposema mkuu wa nchi maana yake Rais anafanya kazi na taasisi mbalimbali wakiwemo awaziri ambao wanamsaidia kazi.

"Dkt.Bashiru katika hotuba yake aliyoitoa ilikuwa haina hoja ya kujibu wakati yeye amekuwa kwenye hiyo kamati ya kilimo...unaporopoka maana yake Serikali unaivua nguo, serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita, jambo ambalo ni la hovyo kabisa."

Amesema, ndani ya Chama Cha Mapinduzi amedumu kwa zaidi ya miaka 19 huku akiwa na kadi ya uanachama Aa977797 ingawa hana uhakika na kadi ya uanachama wa Dkt.Bashiru.

"Dkt.Bashiru alitoa maneno ambayo hayakuwa na lengo la kuimarisha mustakabali wa nchi yetu katika hotuba yake.Yeye alikuwa na muda mrefu ndani ya chama, kama angekuwa na jambo angeweza kusema sio...maneno yake hayo.

"Tunashuhudia bajeti ya kilimo imepanda kutoka shilingi Bilioni 4 hadi Bilioni 400 kama angekuwa na jambo angetoa ushauri na sio kwenda....

"Sote tunashuhudia Waziri Bashe anachapa kazi katika Wizara ya Kilimo amekuwa akigawa matrekta, hii yote ni kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija kwa Watanzania..."

"Usalama wa nchi yeyote ile ni usalama wa chakula na ndio maana Waziri na Serikali inapambana kuhakikisha kilimo kinasaidia kukuza maendeleo...

"Ukija kwenye principles za chama, ibara ya 8 ya nyongeza ibara ndogo ya (v) inasema nitasema ukweli daima, kwangu fitina mwiko.

"Sina mashaka na kauli ya Dkt.Bashiru ila nia yake aliyokuwa nayo nasema kwamba imekwama kutokana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta mbalimbali.

"Wana CCM wanafahamu fika nimepambana na upinzani Kigoma, lengo ni kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani na jambo hili lilifanikiwa...leo hii Bashiru anakuja na hoja ya ajabu kabisa ambayo ki-ukweli hafai.

"Bashiru nia yake ilikuwa kushughulika na makada wote wa CCM. Mnakumbuka uchaguzi wa 2017 makada wote ambao tulikuwa hatununuliki alitushughulikia sana. Pia alitaka tusipate elimu leo hii tumesoma na tunafanya kazi ya chama kwa ufanisi mzuri kabisa.

"Dkt. Bashiru alifukuza makada wenzangu 15 ambao walikuwa wapambanaji ndani ya chama kwa nia ovu kabisa. Tokea nasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Wazalendo wa CCM yeye alikuwa ananinyooshea kidole sana. Alikuwa anaandika ilani ya CUF na alikuwa ameajiriwa kama Mkurugenzi wa Uandishi wa Ilani ya CUF hakuwa mwana CCM.

"Wakati anapata uteuzi wake niliongea na rafiki yake mmoja akaniambia huyu amepata kazi tu, hana lolote siku mkizinguana ataondoka atakuwa amejifunza kwenu sio mwana CCM...

"Mimi nina nia njema ya kusaidia chama changu na sirubuniki na namheshimu Mungu, simuonei Dkt. Bashiru aliwaandikia barua na kuwafukuza kazi makatibu 80. Na pia aliwahi kutamka mimi sifai kuwa kiongozi kwa sababu ya fitina zake.

"Alikuwa na nia ya kushughulika na viongozi waliokifia chama na alifanikiwa kufukuza makada wenzangu 15 kwa kuwaonea kabisa.

"Nampongeza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo walifanya kazi kubwa na Mheshimiwa Mwenyekiti Rais Samia kwa kuhakikisha makada ambao walikuwa nje ya chama wanakuja kukitumikia Chama Cha Mapinduzi.

"Mpango wa Dkt. Bashiru ni kutaka kuifanya CCM iwe dhaifu, ikiondoka CCM tutaumia sisi, binafsi ninaishi kwenye misingi ambayo CCM imerithi kutoka TANU siwezi kukaa kimya kuona Bashiru akiropoka maneno ya hovyo juu ya Chama Cha Mapinduzi.

"Nampongeza Katibu Mkuu kwa hatua ambazo amefanya kuchukua hatua kwa mikoa mitatu ambayo ilionesha nia ya rushwa kuhakikisha chama kinadumu katika misingi yake thabiti na kinaendelea kuwa mfano bora.

"Bashiru alikuwa na nia ovu sana, niwapongeze wana CCM ambao walimkataa Bashiru. Sisi wana CCM tutaendelea kukifia chama na wanaotabiri kina wakati mgumu mwaka 2025 wanajidanganya sana CCM ni chama imara, thabiti kinajipambanua, kimejengeka na kimeimarika.

"Dkt.Bashiru na...lake walikuwa na nia ovu sana na ndio maana walikuwa wanafukuza makada. Ni wajibu wa kila mwana CCM kukisemea chama,"amefafanua Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Augustino Matefu.

Matefu ameendelea kufafanua kuwa, “Hatutakuwa tofauti na mawakala wao wanaowapambana wakati mwingine kuwadanganya kwamba unaupiga mwingi.

"Lakini nasema kitu kimoja chenye pointi ya msingi sana, mfumo wa chama chetu kwenye transition period kila kiongozi anakuwa na maono yake na dira yake ya uongozi.

"Mheshimiwa Hayati Magufuli aliamini katika misingi ya kupata watu ambao hawafungamani asilimia 100 ili apate timu ya uongozi anaoutaka yeye, sisi tunamheshimu kama Mwenyekiti wetu aliyetangulia mbele ya haki.

"Siwezi kusema ametukosea, lakini yeye kwa utashi wake ndio maana huwa tunasena kipindi cha nyuma zidumu fikra za Mwenyekiti kwa hiyo by then fikra za Mwenyekiti zikidumu kwa sasa tumegundua mistakes zilifanyika na yeye mwenyewe alikiri mistake zile wakati anazindua stendi ya Mbezi Luis.

"Wewe Bashiru ni mtu mzuri sana ila niliambiwa wewe ni mtu wa CUF, nitakutafutia majukumu mengine alikuja akarealize yale ambayo tulikuwa tunamweleza.

"Kwa sababu mwanadamu kufanya makosa ni jambo la kawaida, unapofanya makosa unakua na kujiimarisha zaidi na kuwa mzuri tofauti na ulivyokuwa awali kwa hiyo mheshimiwa Magufuli alikuwa na ukada wa staili yake, lakini by then chama chake huwa kina mfumo wake, kwenye mfumo wa kupokezana madaraka.

"Tunaamini kila mwenyekiti anakuwa na maono yake, kwa hiyo sisi tunachofanya tunabariki maono ya Mwenyekiti na ili aweze kufanya kazi sawa sawa na kufika kule anakotaka kufika na kazi ya kwanza ya kufanikisha safari yake afike salama ni kumshauri.

"Na kumshauri kuna mambo mawili, alichue jambo na kulifanyia kazi au aliache jambo kama akiba kwa baadae alifanyie kazi, alijitambua alikosea akasahihisha makosa yake kwa kumteua kwa nafasi nyingine na kumteua mtu mwingine kuendelea na kazi hiyo ya ukatibu mkuu anayefiti kwenye hiyo nafasi na ni kada ambaye hahongeki, hashawishiki. Tumemtawaza sisi ni daktari wa siasa Chongolo.

"Kwa hiyo tusema kwa upande wetu sisi hatujasema alifanya makosa ila yeye alitambua amefanya makosa kwa sababu ndiye alikuwa na maono apeleke CCM awe na CCM ya mfumo upi katika uendeshaji kwa sababu sisi Mwenyekiti anapoingia anakuwa na maono yake,"amefafanua Matefu.

Post a Comment

0 Comments