Majaji wapewa 'kiburi' Afghanistan

NA DIRAMAKINI

KIONGOZI Mkuu wa Afghanistan,Hibatullah Akhundzada amewataka majaji kutekeleza kikamilifu vipengele vyote vya sheria ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na kunyongwa hadharani, kupigwa mawe na kupigwa viboko ikiwemo kukatwa viungo vya mwili wezi.

Msemaji Mkuu wa Kundi la Taliban, Zabihullah Mujahid alituma ujumbe kwenye Twitter yake jioni ya Novemba 13, 2022 akieleza kuwa, amri ya lazima ya Hibatullah Akhundzada ilikuja baada ya kiongozi huyo msiri kukutana na kundi la majaji.

Akhundzada, ambaye hajapigwa picha wala kuweka picha hadharani tangu Wataliban warudi madarakani mwezi Agosti mwaka jana, anatawala kwa amri kutoka Kandahar.

Taliban waliahidi kufanya mabadiliko ya utawala mkali ambao ulidhihirisha nafasi yao ya kwanza madarakani, kuanzia 1996-2001, lakini hatua kwa hatua wamebana haki na uhuru.

"Chunguzeni kwa makini mafaili ya wezi, watekaji nyara na waasi. Hayo mafaili ambayo masharti yote ya sharia (sheria ya Kiislamu) ya hudud na qisas yametimizwa, mnawajibika kuyatekeleza.Hii ni hukumu ya sharia na amri yangu ambayo ni wajibu,"Mujahid alimnukuu Akhundzada akisema ingawa hakupatikana kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu maelezo hayo.

Post a Comment

0 Comments