Rais Dkt.Mwinyi ateta na Konseli Mkuu wa UAE Zanzibar

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar itaendeleza kasi katika kukuza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi Mdogo (Konseli Mkuu) wa Umoja wa Falme za Kiarabu anayefanyia Kazi zake Zanzibar, Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri alipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo Novemba 21, 2022. (Picha na Ikulu).

Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Novemba 21, 2022 Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Saleh Ahmeid Alhemeir aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha.
Ameema, hatua ya nchi hiyo kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar kutatoa msukumo katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ilioanzishwa pamoja na ile inayolengwa kuanzishwa siku za usoni.

Amesema, ni matarajio yake kuwa kupitia Konseli Mkuu Alhemeir, miradi mbalimbali inayotekelezwa na nchi hiyo kupitia taasisi na mashirika ya fedha ya nchi hiyo itafanikishwa.
Naye Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Zanzibar, Saleh Ahmeid Alhemeir amesema hatua ya UEA kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar itaongeza kasi ya ushirikiano na hivyo akaahidi kufuatilia miradi mbalimbali mbayo nchi hiyo imelenga ikisaidia Zanzibar.

Aidha, amesema atahakikisha anasimamia kikamilifu ujenzi wa ofisi za Ubalozi mdogo wa nchi hiyo hapa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news